Kwahiyo Jumamosi Tar 1 September 2012
Baada ya kuamka saa 8 mchana, kukawa na shughuli za kuweka mwili safi
na kuangalia maswala mengine ya kinyumbani ambayo ni ya kawaida kawaida.
Maji kama ilivyo ada lita na nusu
Jioni mida ya saa moja nikawa na miadi ya mtoko na Swahiba wangu wa siku nyingi Dorothy
Tulienda Dinner, Thai Village
Chakula cha ki Thailand. Hakina mafuta mengi.
Kwahiyo tukajiachia hapo weeee na mbili tatu kisha usiku ukawa mrefu.
Yalioendelea yalipelekea kuamka kesho yake Jumapili saa moja Usiku. Tuyaache
Wanaofatilia mlo wanatakiwa kujua tu kuwa Jumamosi nilikula mlo mmoja tu wa usiku
Ambao Ilikuwa ni kuku iliopikwa kwenye sauce na Mboga mboga na Pilipili
Ujazo huo Pamoja na Egg fried Rice
Alivyokula Dorothy tumuachie mwenyewe
Ila hicho kibakuli cha Wali tuli share wote wawili
Usiku huo hakukuwa na haja ya SHAKE OFF maisha tuliokula yenyewe ni SHAKE OFF tosha.
Jumapili Tar 2 September 2012.
Nilikuwa nimelala siku nzima, kwahiyo sijala ila ilikuwa nikistuka usingizini nakunywa maji
Zikafika lita 3, kuamka ilikuwa saa moja jioni
Nikajiandaa nikaenda kazini, Usiku huo nilikunywa Supu ya Kuku tu "Robo Kuku"
Jumatatu tar 3 September 2012
Kuamka ni jioni saa kumi
Muda wa mlo ni saa kumi na mbili jioni
Samaki wa kuchemsha mkubwaa, na Vegies na Fresh Juice
Jumanne Tar 4 September 2012
Kuamka mapema saa 4, kuzunguka katika shughuli zangu za kila siku
Sikula siku nzima na nililala hivyo hivyo
Nilikunywa maji tu siku nzima, sikumbuki ujazo kiasi gani ila najua ni maji mengi tu ya kutosha.
YESU alikaa siku 40 na hakufa!!
Kwahiyo siku 1 tu haina madhara yoyote ku skip mlo
Jumatano Tar 5 September 2012
Kuamka saa 4 Asubuhi, kazi za hapa na pale
Lunch saa saba mchana Dagaa vijiko 3, Spinach kiduchuu, Firigisi 4, Ndizi nusu "Bukoba" Wali Vijiko 10
Fresh Juice glass 1
Baada ya hapo maji mpaka nalala
Tukutane tena siku zijazo, kuanzia Alhamis
Hicho chakula picha ya chini kinapatikana Nyumbani Lounge
4 comments:
yaani hiyo misosi nikiiangalia yaani inavutia mnooooooooo
Ungeniambia shake off mapema nikabeba vi roba vyangu lol! msosi kwa kweli unavutia sana. Asante kwa ushirikiano wako.
Misosi inavutia sanaa asante kwakushare lol
ILA JIDE UNAONA UNAVYOWAFUNDISHA WATU WAFUATE DIET YAKO NISAWA KWELI?MAANA MARA WANYWA BIA SIKUINGINE.MARA WAKAA SIKUNZIMA BILA KULA KABISA JE NI DIET GANI HII NANIYA WAPI ,MIE NIKO SWEDEN NA NILISHA KATAZWA KABISA NA MAMA WAKISWEDE YAANI BOSS WANGU ALINIONYA KUACHA KULA KABISA SIO VZURI NA WALA DIET HAIFANYWI KIHIVYOO NIMBAYA SAANA ,UNACHOTAKIWA UWE NA POSSION SIZE YACHAKULA.NAPIA UANGALIE VITU UNAVYOKULA SIO KUFAKAMIA KILA KITU.BIA ,SODA COCA UACHE KABISA,NAHAPANILIPO UKINIONA NIMEKATA KASHEPU KAZURII SAAANA NITAKUTUMIA PICHA YANGU NA FULL DIET PIA IF IS OK 4 U JIDE.OTHER WISE BARIKIWA NA YESU.
Post a Comment